The House of Favourite Newspapers

Apple kuinunua Tidal ya Jay Z

0

heres-what-students-learn-in-a-college-course-on-kanye-west-and-jay-zs-relationshipMarekani

KAMPUNI ya teknolojia ya Apple nchini Marekani inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja kutoka Kapuni ya Tidal inayomilikiwa na mwanamuziki maarufu duniani Jay Z .

Apple imeripotiwa kwamba inataka kuinunua Tidal kutokana na ushirikiano wake na wanamuzika bingwa kama vile Kanye West na Madonna ambao wanafanya kazi za kimuziki na Tidal.

Beyonce-Jay-Z-Best-PDA-Moments-Pictures.jpgJarida la Wall Street limechapisha taarifa kuwa mazungumzo yameanza kati ya wamiliki wa makampuni hayo mawili na huenda makubaliano yakafikiwa hivi karibuni na hatimaye biashara kufanyika. Wakati taarifa hizo za Wall Street zikisambaa, Msemaji wa Tidal amekana kufanya mazungumzo na Apple.

Jay Z alizindua huduma hiyo Machi 2015 kama mpinzani wa Spotify baada ya kununua Kampuni ya kiteknolojia ya Sweden, Aspiro ambayo ilikuwa ikiimiliki Tidal kwa takriban dola milioni 56.

Wadeau wengine kwenye Kampuni ya Tidal mbali na Jay Z ni mkewe, Beyonce, rapa Kanye West na Alicia Keys.

Leave A Reply