The House of Favourite Newspapers

Arsenal Yatinga Nusu Fainali Carabao Cup

0

Washika mitutu wa London, Arsenal wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Sunderland usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London.

Shujaa wa Arsenal jana alikuwa ni mshambuliaji Eddie Nketiah aliyefunga mabao matatu peke yake dakika za 17, 49 na 58, wakati mabao mengine yamefungwa na Nicolas Pepe dakika ya 27 na kinda wa umri wa miaka 18 aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza, Charlie Patino dakika ya 90+1.

Mechi nyingine tatu za hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Carabao Cup zitapigwa leo.

Leave A Reply