The House of Favourite Newspapers

Ashambulia chuo na kuua watu 9 Marekani

0

Mauaji Oregon (10)

Mmoja wa majeruhi katika shambulio la Oregon akipatiwa huduma ya kwanza.

Mauaji Oregon (7)

Muuaji wa watu tisa katika shambulio hilo, Chris Harper-Mercer, 26, enzi za uhai wake.
Mauaji Oregon (2)

Mauaji Oregon (3) Mauaji Oregon (4)

Baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi wa Umpqua wakiwa na sintofahamu baada ya kutokea shambulio hilo.

Mauaji Oregon (5) Mauaji Oregon (6)

Waombolezaji wakiwa na simanzi baada ya shambulio la jana.
Mauaji Oregon (9)
Mauaji Oregon (11)Wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Umpqua jimboni Oregon nchini Marekani wakikaguliwa wakati wakitoka chuoni hapo.

WATU tisa wameuawa na wengine saba kujeruhiwa baada ya kijana mmoja kushambulia kwa risasi katika Chuo kimoja kilichopo Roseburg jimboni Oregon, Marekani jana.

Kijana huyo aitwaye Chris Harper-Mercer, 26, akiwa na silaha alifyatua risasi kwenye Chuo cha Umpqua na kuua watu tisa kisha na yeye kuuawa wakati alipokuwa akijibizana kwa risasi na polisi.

Sababu za muuaji huyo kutekeleza shambulio hilo bado hazijajulikana, ingawa polisi wanasema wanafanyia uchunguzi ripoti kuwa alitahadharisha dhamira yake hiyo katika mtandao wa kijamii.

Saa kadhaa baada ya shambulio hilo, ambalo watu saba walijeruhiwa, Rais wa Marekani, Barack Obama ametaka kuwe na sheria kali za udhibiti wa silaha.

Leave A Reply