The House of Favourite Newspapers

AUBAMEYANG Augua Malaria

0

Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ametibiwa hospitalini baada ya kuugua malaria wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa na Gabon.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga BAO katika ushindi wao wamabao 3-0 wa Gabon dhidi ya DR Congo katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika, Machi 25, 2021.

 

Aliichezea Arsenal katika mchuano wao wa Kombe la Europa dhidi ya Slavia Praguetarehe Aprili 8, lakini alikosa mechi dhidi ya Sheffield United siku ya Jumapili ambapo Arsenal ilishinda.

 

“Nimekuwa hospitalini kwa siku chache wiki hii. Ninahisi nafuu kila siku kwa msaada wa madaktari bora waliogundua na kunitibu haraka….’ alisema kupitia Instagram. 

 

Leave A Reply