The House of Favourite Newspapers

Aunt ajivunia penzi la Moze Iyobo

0

aunty33Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moze Iyobo.

Musa mateja
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema hakuna kitu ambacho anajivunia maishani kama kupewa penzi motomoto na mpenzi wake, Moze Iyobo.

Akipiga stori hivi karibuni na paparazi wetu, Aunt Ezekiel aliweka wazi kwa kusema kwamba anajivunia kuwa na Iyobo kwani ni mwanaume sahihi kwake na amekuwa akimfanya kuwa na furaha muda wote.

“Najisikia raha sana kuwa na Iyobo wangu na ndiyo maana utaona kila sehemu nafuatana naye, hana makuu ingawa katika maisha kukwaruzana kupo ila yeye ni mstahimilivu kupita maelezo, naweza kusema tangu niyajue maisha ya mapenzi, Moze ni mwanaume ambaye nimeishi naye kwa amani na upendo hivyo naomba Mungu aendelee kunijalia zaidi tutimize ndoto zetu,” alisema Aunt Ezekiel.

Leave A Reply