The House of Favourite Newspapers

Auza Nywele Zake Apate Pesa ya Kulisha Watoto

0

MWANAMKE mmoja kutoka nchini India ameamua kuuza nywele zake ili aweze kupata chakula kwa ajili yake na familia yake, jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa jamii yake.

 

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Prema Selvan, (31) anayeishi eneo la Salen mji wa Tamil Nadu, amesema mwanaye Kaliyappan mwenye umri wa miaka saba alirudi kutoka shuleni na kumuomba chakula kisha kaanza kulia kwa sababu ya njaa jambo ambalo lilimuuma sana, lakini hakuwa na kitu chochote cha kuuza ili apate pesa ya chakula.

Prema anasema alilikumbuka duka ambalo alikuwa akiona wakiuza nywele ndipo alipoamua kwenda kuuza nywele zake zote kichwani kwa rupia 150 ($2).

Nywele za kubandika za binadamu huuzwa kote ulimwenguni na India ndiyo inayouza kiwango cha juu cha nywele hizo nje ya nchi.

Leave A Reply