The House of Favourite Newspapers

Aweso: Tumekwamua Miradi ya Maji Kichefuchefu 142 Kati ya 177

0

MBOZI-SONGWE

WAZIRI wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa mkoani Songwe ametoa taarifa maalumu juu ya mageuzi makubwa yaliofanyika katika kukwamua miradi mingi iliokwama kipindi cha nyuma na kuchafua taswira ya sekta ya Maji.

Akiwa Mkoani Songwe kwenye kikao na Watumishi wa sekta ya Maji Waziri Aweso amesema.

“Tulipoanzisha Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira vijijini RUWASA July 2019 na kuanza kusimamia utekelezaji wa miradi ya Maji vijijini chini ya Wizara ya Maji tulipokea Miradi yenye changamoto ambayo tuliipa jina la “MIRADI KICHEFUCHEFU jumla ya 177 toka Halmashauri mbalimbali, ni faraja kubwa kwetu mpaka sasa tumekwamua jumla ya Miradi 142 ambayo ina ubora, inafanya kazi na wananchi wanapata Maji.

Aidha Mkoa wa Songwe pekee ulikua miradi kichefuchefu 19 iliopokelewa toka Halmashauri na hadi sasa imekwamuliwa yote ikiwa miwili ipo hatua za mwisho.

Leave A Reply