The House of Favourite Newspapers

Azam FC Wafungukia Ndege Yao

KUPITIA kwa meneja wa Azam FC, Philipo Alando, hatimaye amefungukia gumzo la ndege yao iliyoonekana ikiwashusha baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kwa kusema kuwa ndege hiyo siyo mali ya timu bali ni mali ya Makampuni ya SSB.

 

Azam juzi ilikwenda kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kuvaana na Kagera Sugar ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Alando alisema kuwa watu wamezungumza mengi sana juu ya ndege hiyo lakini ukweli ni kwamba hiyo ndege siyo mali ya timu bali ni mali ya kampuni ya SSB ambayo ndiyo kampuni mama.

 

“Hiyo ndege haina uwezo wa kubeba timu nzima hivyo inabeba abiria 13 tu, kwa sababu ni mali ya kampuni kwa ajili ya mambo mbalimbali ya viongozi wetu, juzi ilitakiwa kuja Bukoba kwa nia ya kuwaleta baadhi ya viongozi na lengo jingine likiwa ni kurudi na baadhi ya wachezaji wa timu za taifa ili wawahi kuripoti maana tulijua kurudi na basi kwa pamoja wangeweza kuchelewa kuripoti kambini,” alisema Alando.

Musa Mateja, Dar es Salaam

FATMA KARUME – “Makonda Anakurupuka, Adui Sio Ushoga”

Comments are closed.