Azam FC waitana, wamjadili Makambo

VIGOGO wa Azam FC wametishwa na fomu ya Yanga ya kushinda mechi zao licha ya kwamba wako ‘unga’ kiuchumi, hivyo Jumatatu walikaa kikao kwa ajili ya kuwajadili akiwemo straika wao, Heritier Makambo anayeongoza kwa mabao katika kikosi hicho.

 

Azam FC wanaofundishwa na kocha Iddy Cheche aliyepokea kijiti kutoka kwa Hans van Pluijm, Jumatatu ijayo watakuwa wanapambana na Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara.

 

Mratibu wa Azam FC, Philipo Alando, amesema kwamba Jumatatu ya wiki hii kocha na wachezaji walikaa kwa ajili ya kujadili juu ya mchezo huo na kupeana majukumu.

 

“Mechi hii ni ngumu na muhimu kwetu lakini pia kwa wapinzani wetu. Jumatatu tulikaa na kupeana majukumu juu ya nini tutakifanya kwenye mechi hii.

 

“Ilikuwa ni saa chache baada ya wachezaji kurudi kambini, wakitokea kwao walipoenda kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka. Tulikaa na kukumbushiana juu ya umuhimu wa mechi hii dhidi ya Yanga,” alisema Alando.

Loading...

Toa comment