The House of Favourite Newspapers

Azam yakiri Yanga kiboko

0

Said Ally,
Dar es Salaam
INGAWA kikosi cha Azam kinaongoza katika msimamo wa ligi kuu kikiwa na pointi 25, kocha mkuu wa timu hiyo, Muingereza, Stewart Hall, ametamka kuwa hawezi kutamba kwa kukaa katika nafasi hiyo kwa sasa kutokana na ushindani kuwa mkubwa baina yao na Yanga ambao wapo katika nafasi ya pili.

Azam kwa sasa ndiyo vinara wa ligi baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Toto Africans kwa mabao 5-0, ambapo wananyemelewa kwa ukaribu na Yanga walio kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 23.
Akizungumza na Championi Jumatano, Stewart alisema kuwa hawawezi kuanza kushangilia kukaa kileleni kwa sasa kutokana na ligi kuwa bado mbichi.
“Hatuwezi kuanza kujisifu kwa kuwa tupo kileleni kwa sasa wakati ligi yenyewe ndiyo kwanza mbichi, tena tukicheza mechi tisa pekee, labda ingekuwa mechi 28 kidogo hapo tungestahili kujipongeza.
“Lakini kwa sasa tunatakiwa kujituma zaidi katika michezo yetu inayokuja kwani wapinzani wetu, Yanga wamekuwa wakitupa presha ya hali ya juu kutokana na wao kutaka kurejea katika nafasi hii tuliyopo sisi.
“Na utaona kama tukifanya uzembe katika mchezo wetu mmoja tu basi kila kitu kitabadilika ila kikubwa ambacho nawaagiza wachezaji wangu ni kuhakikisha tunaibuka na pointi tatu katika kila mchezo wetu ule, haijalishi hata kama una ugumu kiasi gani,” alisema Stewart.

Leave A Reply