Baada ya Tanasha, Warembo Wapangwa Foleni kwa Mondi

DAR: “Mnataka Simba apate demu nchi gani?” Swali hilo la msanii wa Bongo Fleva anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ alilouliza kupitia ukurasa wake wa Twitter mapema wiki hii, limesababisha warembo wakali barani Afrika kupangwa foleni kwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Swali hilo la Rayvanny linakuja wakati kukiwa na vuguvugu la madai ya Diamond au Mondi kuachana na mzazi mwenzake, Tanasha Donna tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, hivyo warembo mbalimbali wanatajwa kuwa wanafaa kuchukua nafasi hiyo.

 

Tayari Mondi amezaa na wanawake tofauti kutoka nchi tatu za Afrika Mashariki. Kufuatia swali hilo, mashabiki wengi wa Mondi ndani na nje ya Bongo, walianza kutoa maoni yao ambapo warembo kama Dillish Mathews (Namibia), Nadia Buari na Juliet Ibrahim (Ghana), Faith Nketsi (Afrika Kusini), Toke Makinwa (Nigeria) na wengine kadhaa.

 

Baada ya bandiko hilo la Rayvanny, Gazeti la IJUMAA limefuatilia uchambuzi na ni nani anayefaa kumrithi Tanasha ambapo mitandao mbalimbali ya burudani barani Afrika, iliwataja warembo na sifa ambazo zinawabeba warembo kadhaa wakali wanaopigiwa chapuo kwa Mondi.

 

LENGO KUKUZA HIMAYA KIMUZIKI

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari za burudani barani Afrika ikiwemo Kenya, Nigeria na Ghana, Mondi anaaminika kuwa, yupo mbioni kusaka mrembo kwenye Taifa lingine nje ya Tanzania, Kenya na Uganda, lengo likidaiwa kuwa ni kukuza zaidi himaya yake kimuziki.

 

“Kuna kitu watu wengi hawakijui, Mondi anatumia wanawake hasa wenye majina kwenye nchi zao kujipatia mashabiki kwenye nchi au ukanda husika,” alieleza mmoja wa wachambuzi wa habari za mastaa nchini ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Mondi katika mazungumzo na mwandishi wetu.

 

Shabiki huyo alieleza kuwa, kutoka kwa Wema Sepetu, Jacqueline Wolper na wengine wengi (mastaa wa filamu za Kibongo) waliompa mashabiki wengi kisha Hamisa Mobeto, (mwanamitindo maarufu Bongo), Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, staa wa Uganda na baadaye Tanasha (video vixen na mtangazaji maarufu Kenya), kote huko Mondi alivuna mashabiki lukuki.

 

Swali la msingi linaloulizwa, ni je, ataibukia taifa gani barani Afrika?

Kwa mujibu wa mitandao mikubwa ya burudani barani Afrika, baadhi ya warembo wenye majina makubwa nchini mwao wanaoaminika kuwa Mondi anaweza kuibuka huko ni hawa wafuatao;

 

TOKE MAKINWA (NIGERIA)

Mitandao hiyo inaeleza kuwa, kama ilivyokuwa kwa Tanasha, Toke ni mtangazaji na video vixen maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti). Mwaka 2010 alishinda Taji la Miss Nigeria. Amejaaliwa umbo matata linalomfanya ‘ku-trendi’ mitandaoni.

 

Ilieleza kuwa, Toke aliwahi kuolewa na Maje Ayida, lakini ndoa yao haikudumu hivyo yupo ‘free’ hivyo kama Mondi anataka kuendelea kutisha nchini Nigeria na Afrika Magharibi, Toke ndiye mrembo sahihi kwake.

 

FAITH NKETSI (AFRIKA KUSINI)

Mitandao hiyo ilieleza kuwa, Faith ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Afrika Kusini akiwa na sifa ya kuwa na zigo (kalio) linaloondoa utulivu kwa baadhi ya wanaume wanaopenda mambo hayo.

Ni video vixen matata ambaye ameuza nyago kwenye video za mastaa wakubwa kama Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.

 

Ilielezwa kuwa, kuna kipindi mrembo huyo alidaiwa kutoka kimapenzi na staa wa muziki wa Nigeria, Davido baada ya kuvuja picha zao za kimahaba wakiwa kitandani.

Ilielezwa kuwa, kwa ukubwa wa jina lake kwenye ‘showbiz’ (biashara ya shoo) nchini Afrika Kusini na barani Afrika, Faith anaaminika kuwa chaguo sahihi kwa Mondi.

 

JULIETH IBRAHIM (GHANA)

Mitandao hiyo inamtaja Julieth kuwa kinara wa filamu nchini Ghana (Gollywood) akiwa na umbo lake matata kwenye mitandao ya kijamii. Pia ni prodyuza wa filamu na ni mwanamuziki maarufu nchini humo.

Ilisemekana kuwa mrembo huyo aliwahi kuolewa, lakini akapewa talaka kisha akadaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa Nigeria, Iceberg Slim kabla ya kumwagana mwaka jana.

 

Kama alivyo Tanasha, Juliet ni chotara ambaye ni mchanganyiko wa Mliberia na Mghana. Kama ilivyokuwa kwa Zari aliyekuwa ameolewa na tajiri maarufu nchini Uganda, Ivan Ssemwanga’ kabla ya kuachana na kutua kwa Mondi, Julieth naye alikuwa ameolewa na tajiri wa nchini Ghana, Kwadwo Safo Jnr.

 

Inaaminika kuwa, akili ya biashara ya muziki wa Mondi, ikiunganishwa na ya Julieth, basi Mondi atajenga himaya nyingine ya muziki wake nchini na Nigeria na ukanda wa Afrika Magharibi. Kuna maelezo kwamba, Ghana ni moja ya nchi ambazo Mondi anataka kujenga himaya yake kimuziki.

 

NADIA BUHARI (GHANA)

Mitandao hiyo inamtaja Nadia kuwa mmoja wa waigizaji wenye majina makubwa nchini Ghana (Gollywood). Mbali na uigizaji, pia ni mrembo matata ‘anaye-trendi’ kwenye mitandao ya kijamii. Ana ‘ugonjwa’ wa Mondi kwani anavutiwa na mambo hayo.

 

Pamoja na kwamba ana umri mkubwa, inadaiwa kwamba siyo kigezo cha Mondi kutokumuweka kwenye ‘tajeti’ yake kwani ana umri sawa na Zari ambaye jamaa huyo alishazaa naye watoto wawili.

Nadia aliwahi kusemekana kutoka kimapenzi na staa wa soka wa nchini kwake, Ghana, Michael Essien aliyewahi kuichezea Timu ya Chelsea ya Uingereza kabla ya kudaiwa kuwa ‘singo’.

Nadia anatajwa kuwa na vigezo vingi vinavyoweza kumfanya Mondi kupanda ndege na kumfuata nchini Ghana.

 

SHADDY BOO (RWANDA)

Kwa mujibu wa mitandao hiyo, Shaddy aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Mondi, lakini ishu hiyo ilizimwa kiaina.

Ni bonge la video vixen na mwenye umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) kutokana na umbo lake matata.

 

Iliibuka minong’ono mingi baada ya kusambaa kwa picha zake akiwa na Mondi hotelini huko Kigali nchini Rwanda mwaka 2018.

Mwaka 2018, Shady alitua Bongo kwa ajili ya kusimamia Kipindi cha Wasafi TV cha Jibebe Challenge chini ya Mondi ambapo ilisambaa picha akiwa kitandani na jamaa huyo wakiwa wamejifunika shuka nyeupe, hivyo lolote linawezekana.

 

DILLISH MATHEWS (NAMIBIA)

Inaelezwa kuwa, wakati Mondi akiachana na Zari, kulikuwa na tetesi za kimapenzi juu ya jamaa huyo na mrembo huyo wa Namibia ambaye aliibukia kwenye Shindano la Big Brother Africa.

Pia mrembo huyo aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa soka wa Togo, Emmanuel Adebayor aliyewahi kutisha na timu mbalimbali nchini Uingereza ikiwemo Arsenal.

 

Kuna kipindi Dillish aliwahi kunaswa na Mondi visiwani Zanzibar wakila bata, lakini tetesi hizo zilizima ghafla.

Dellish ni mwigizaji mkubwa nchini Namibia, ana umaarufu mkubwa Afrika Kusini na Afrika Magharibi akifanya kazi na wasanii wengi wa Nollywood nchini Nigeria.

Kama Mondi akiamua ‘kurejesha majeshi’ kwa Dellish basi ana uhakika wa kujizolea mashabiki wengi wa mrembo huyo mwenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

 

FAMILIA INA ‘MTU WAO’

Wakati hayo yakiendelea kwenye mitandao ya burudani, kwa mujibu wa vyanzo ndani ya familia ya Mondi vilivyozungumza na gazeti ndugu la hili la Risasi Mchanganyiko, familia ya Mondi, yenyewe ina jina la ‘mtu wao’.

Vyanzo hivyo, vinaeleza kuwa, familia hiyo inamkubali mrembo kutoka Uarabuni kwenye familia ya kifalme nchini Oman.

Stori: MWANDISHI WETU, Ijumaa

Toa comment