The House of Favourite Newspapers

Baadhi ya Hoteli za Ngurdoto Kupigwa Mnada Kulipa Madeni

0

MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha masjala ndogo ya kazi imeamuru baadhi ya mali za Hotel ya Kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo eneo la mji mdogo wa Usariver Wilayani Arumeru Mkoani Arusha zikamatwe kwa ajili ya kupigwa mnada kufidia mishahara ya waliokuwa wafanyakazi 93 wa Hoteli hiyo wanadai kiasi cha Tsh. Milioni 129.

Naibu msajili wa Mahakama hiyo John Nkwabi alitoa maamuzi hayo jana katika mahakama Kuu kanda ya Arusha masjala ndogo ya Mkoa katika kesi ya msingi namba 140 ya mwaka 2020, ya madai ya waliokuwa wafanyakazi 93 dhidi ya mwajiri wao Hotel ya Ngurdoto Mountain Lodge.

Kesi hiyo iliyosajiliwa oktoba 16 Mwaka 2020 iliendeshwa katika hatua mbalimbali na kufidia tamati jana ambapo Msajili Nkwabi kwa kuzingatia sheria za kazi alitoa hukumu ya kukamatwa ili baadae zipigwe mnada kwa baadhi ya mali za Hoteli hiyo ili kupata kiasi cha shilingi 129,570,000 za kuwalipa madai ya mishahara ya wafanyakazi hao.

Nkwabi alitaja mali hizo kuwa ni vitanda 139, Gari aina ya Coaster bus lenye namba za usajili T847 DPH, kiwanja namba 418 kilichopo Block A eneo la Leganga, Usariver, Arusha na mashine nne za nguo za kufulia.

Msajili huyo alimuagiza dalali Allan Mollel wa kampuni ya udalali ya “First World Investment Auctioneers Debt” ya jijini Arusha kukamata mali hizo mara moja ili kusubiri amri ya mahakama tarehe 4.5.2021 kwaajili ya kuuzwa kufidia mishahara ya wafanyakazi.

Pamoja na mahakama waliondesha shauri hilo mahakamani ni Ofisa kazi mfawidhi wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha kwa niaba ya Kamishna wa kazi dhidi ya upande wa uatetezi wa wakili Edmund Ngemela.

Leave A Reply