The House of Favourite Newspapers

Shigongo Alivyosimama Bungeni, Kuwasilisha Maoni Ya Kamati Ya Bunge -Video

0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira, Eric Shigongo, akiwasilisha Bungeni ripoti ya kamati hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Eric Shigongo, leo Aprili 27, 2021 amewasilisha Bungeni ripoti ya kamati hiyo, katika Bunge la 12, mkutano wa 3, kikao cha 17.

 

Shigongo ameishauri Ofisi ya Makamu wa Rais ishirikiane na Ofisi ya Mkemia Mkuu kudhibiti uingizwaji wa zebaki nchini. Katika hotuba hiyo aliyoiwasilisha kwa niaba ya Mwenyekiti Mhe. David Kihenzile alishauri Serikali itafute teknolojia mbadala ambayo wachimbaji hao wataitumia ili kuachana na matumizi ya zebaki.

 

“Uingizaji holela na utumiaji wa kemikali ya Zebaki nchini kutokana na kuwapo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wanotumia kemikali hiyo, unaathiri kwa kiasi kikubwa afya na usatwi wa wchimbaji hao. Madhara ya matumizi ya kemikali hiyo yanatokana na wachimbaji wengi kuitumia bila ya kuwa nyenzo za kujinga kutokana na zebaki,” alisema.

…Shigongo akiendelea kuwasilisha ripoti ya kamati hiyo.

Shigongo ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa alitahadharisha kuwa maji yanayotumika kusafishia dhahabu yakiwa yamechanganyika na Zebaki, yanatiririkia kwenye vyanzo vya maji na kuwa watu wanapotumia maji hayo.

 

Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Hawa Mchafu alishauri Serikali itumie fedha kutoka mifuko ya mazingira kwa kusaidia katika kujenga uelewa wa kupunguza matumizi ya zebaki.

 

Pia Mbunge huyo alipendekeza njia mbadala ya matumizi ya zebaki na kusema kuwa kemikali hiyo ina athari kubwa kwa binadamu hususan katika maeneo ya Kanda ya Ziwa ambako kuna shughuli za uchimbaji wa dhahabu.

 

6.6 Matumizi ya kemikali hatarishi – Zebaki

Mheshimiwa Spika, uingizaji holela na utumiaji wa kemikali ya Zebaki nchini kutokana na kuwapo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wanotumia kemikali hiyo, unaathiri kwa kiasi kikubwa afya na usatwi wa wchimbaji hao. Madhara ya matumizi ya kemikali hiyo yanatokana na wachimbaji wengi kuitumia bila ya kuwa nyenzo za kujinga kutokana na zebaki. Vilevile, maji yanayotumika kusafishia dhahabu yakiwa yamechanganyika na Zebaki, yanatiririkia kwenye vyanzo vya maji kama vile mito na mawaziwa. Watu wanapotumia maji kutoka vyanzo hivyo vilivyochafuliwa na zebaki ya kuoshea dhahabu, huathirika kiafya na wakati mwingine kupata maradhi sugu yanayogharimu maisha yao.

 

Mheshimiwa Spika, Kutokana na hali hiyo, Kamati inashauri kuwa:-

  1. i) Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira ishirikiane na Ofisi ya Mkemia Mkuu kudhibiti uingizwaji na zebaki nchini;
  2. ii) usimamizi na uratibu matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini  25 uendelezwe na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa pamoja na Ofisi ya Mkemia Mkuu; na

iii) Serikali itafute teknolojia mbadala ambayo wachimbaji hao wataitumia ili kuachana na matumizi ya zebaki.

 

6.7 Taarifa ya Hali ya Mazingira nchini

Mheshimiwa Spika, Kifungu 175 (1) cha Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kinamtaka Mkurugenzi wa Mazingira kuandaa na kutoa taarifa juu ya Hali ya Mazingira nchini kila baada ya miaka 2 na kuiwasilisha Bungeni. Hata hivyo uzoefu unaonesha kuwa upo ugumu wa kutekeleza masharti hayo jambo lililosababisha kuwasilishwa kwa taarifa hiyo mwaka 2008, 2014 na 2019. Kwa sababu hiyo, taarifa ya kwanza, ya pila na ya tatu hazikuweza kuzingatia masharti ya kuwasilishwa baada ya miaka miwili. Kwa msingi huo, Kamati inashauri kuwa Serikali iandae mapendekezo ya marekebisho ya kifungu hicho kwa kuongeza muda wa kutoa ripoti kufikia miaka 5.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply