Baba mkwe wangu ananitaka kimapenzi!

ANTI Liz, assalaam aleykhum! Ni matumaini yangu kwamba umesherehekea vizuri Sikukuu ya Idd na unaendelea vizuri na kazi.

Mimi ni mwanamke nipo kwenye ndoa na ninampenda sana mume wangu.

Kilichonifanya niombe ushauri wako ni kwamba baada ya kuolewa tunaishi nyumbani kwa baba mkwe wangu ambaye ametupatia upande mmoja wa nyumba yake.

Hapo nyumbani pia yupo baba mdogo wa mume wangu ambaye ameoa na ana watoto wawili, sasa huyo mkwe wangu mara kwa mara amekuwa akinitongoza na kunisifia kwamba mimi ni mrembo sana.

Kwa kuwa ana namba yangu hunitumia ujumbe na mara kadhaa amewahi kunitumia fedha lakini namrudishia. Nahofia nikimwambia mume wangu nitaleta uhasama baina yao, nishauri.

Halima, Dar.

Halima, kwa tabia hiyo ya mkweo huyo ni vyema umuonye kwa ukali na mweleze kama hataacha utamwambia mumeo naamini ataacha.

Jambo lingine la muhimu mwambie mumeo mhame hapo kwa wakwezo na kama mkweo huyo ataendelea kukusumbua liweke wazi kwa mumeo kwani atakuharibia ndoa yako.

 


Loading...

Toa comment