The House of Favourite Newspapers

Hataki tukutane, eti natoa harufu!

0

Couple sitting on sofa with arms folded, looking angryANTI Liz, mimi ni mwanamke niliyeolewa miaka minne iliyopita, naishi jijini Dar es Salaam na mume wangu.

Jambo ninaloomba ushauri wako ni kwamba awali kabla sijajifungua mtoto wetu ambaye hivi sasa ana miaka miwili na miezi mitatu, nilikuwa mwembamba.

Lakini hivi sasa nimekuwa mnene sana kama walivyo shangazi zangu hadi najichukia.

Tangu niwe mnene naona mume wangu amepunguza kasi ya kunihitaji na siku akitaka tule chakula cha usiku huniambia nijipulizie manukato au nipake losheni.

Kutokana na utaratibu huo mpya nilimuuliza kulikoni, bila kumung’unya maneno akaniambia siku hizi natoa harufu ambayo haipendi.

Tangu aliponiambia hivyo nimekosa raha, hivi nakabiliwa na tatizo gani?

Mama P, Dar.

Mama P, kwanza mshukuru mumeo kwa kukuweka wazi juu ya hali yako kwani hivyo ndivyo wanandoa wanavyopaswa kufanya.

Kwa kifupi ni kwamba kunenepa kwako ndiko kunakosababisha hali hiyo hivyo unapooga jisugue vizuri sehemu zenye mikunjo na anza kufanya mazoezi na kuzingatia kula kwa mpangilio utapungua na kuwa kama zamani.

Leave A Reply