The House of Favourite Newspapers

Bahati Nasibu ya Shinda Gari Kupitia Championi Yatikisa Mitaani

0

 

Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Global Publishers, Anthony Adam (kulia) akimkabidhi muuzaji wa magazeti, ndoo kwa ajili ya kuweka na kutunza kuponi za promosheni ya Baba Lao inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra.

NI baba lao, ndiyo wimbo pendwa unaoimbwa hivi sasa katika mitaa na miji yote ya Tanzania, mara baada ya Kampuni ya Global Publishers kupitia gazeti lake la michezo na burudani la Championi kuja na Bahati Nasibu ya kibabe ambayo mshindi atanyakua ndinga mpya aina ya FunCargo.

 

Bahati Nasibu hiyo iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya, inawahusu wasomaji wote wa gazeti la Championi.

 

Lakini mbali na mshindi wa jumla kuchomoka na ndinga, wapo ambao kila wiki watakuwa wanajidai na simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.

 

Kitu bora zaidi katika bahati nasibu hiyo ni kwamba, msomaji wa gazeti la Championi atapata burudani na taarifa konki za kimichezo za ndani na nje ya nchi, kisha mwisho wa yote atajikuta ananyakua ndinga, kwa gharama ya shilingi 800, ambayo ndiyo gharama halisi ya gazeti hilo.

 

Timu ya masoko ya Championi ilizunguka katika mitaa mbalimbali kuitangaza bahati nasibu hiyo huku zawadi mbalimbali za tisheti zikitolewa kwa wananchi waliojitokeza kuipokea habati nasibu hiyo.

Uzinduzi wa bahati nasibu hiyo ilifanyika katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, ulizinduliwa Alhamisi ya wiki iliyopita na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akimuwakilisha rais wa shirikisho, Wallace Karia.

Fainali ya bahati nasibu hiyo itafanyika baada ya miezi mitatu, huku mshindi wa jumla akitarajiwa kujinyakulia Toyota FunCargo mpya, huku wengie wakizoa simu mpya kila siku.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Nyamlani alilipongeza gazeti la Championi kwa kuandika habari za ukweli na za uhakika, huku akitaka wasomaji wote nchini kushiriki shindano hilo ambalo alisema ni kama zawadi kwa Watanzania.

“Kuhusu bahati nasibu, niwapongeze, naamini mnarudisha shukrani zenu kwa jamii ambayo siku zote imekuwa ikiwasapoti katika habari ambazo mnaziandika na wao wananunua magazeti na kuzisoma,” alisema Nyamlani.

 

Anthony Adam, Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers, alisema kuwa bahati nasibu hiyo imeziteka wilaya na mikoa yote ya Tanzania, ambapo amekuwa akipokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa wasomaji, ambao wengi wameahidi kushiriki hadi mwisho.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mhariri Mtendaji, Saleh Ally ‘Jembe’, wameendelea kutoa wito kwa wananchi kusoma gazeti la Champoni kwa kuwa watafaidika na vitu vingi, ukitoa habari na makala ‘Exclusive’, wanaweza pia kujishindia gari ambayo inaweza ikabadili maisha yao.

 

“Tunahitaji wasomaji wetu waweze kujikwamua kiuchumi, ndiyo maana tumetoa zawadi ya gari ambalo naamini kama mshindi atashinda gari hili, ataweza kulitumia kama taksi ama usafiri wake binafsi, hivyo watu wanunue zaidi Gazeti la Championi waweze kujishindia. Championi linatoka Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi na linapatikana kwa Sh 800 tu,” alisema Mrisho.

Kwa upande wa Mhariri Mtendaji, Saleh Ally, alisema: “Championi na Spoti Xtra ndiyo magazeti pekee yenye habari bora zilizojaa takwimu na habari za uhakika hapa nchini, hakuna gazeti ambalo utapata kila kitu isipokuwa Championi na Spoti Xtra.

 

“Lakini pia katika kila shindano au promosheni inayoletwa na magazeti haya, hutoa zawadi za ukweli kabisa tofauti na watu wengine ambao hudanganya, hivyo wasomaji kupitia magazeti haya washiriki na waone jinsi gani watakavyoshinda zawadi kemkem.”

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Leave A Reply