The House of Favourite Newspapers

Balaa la Ngoma ya Nandy, Harmo

0

 

BAADA ya Janga la Corona kupungua makali, wasanii nao wanaanza kurudi kwenye reli tena kama zamani.

Kwani wasanii wengi walikuwa wakitoa ngoma kwa kusuasua sana, wakihofia ngoma zao kutokiki kutokana na janga hilo.

 

Juni hii tayari zimeruka ngoma kali kali ambazo kwa sasa ndizo habari ya Mji wa YouTube, kuanzia So Hot ya King Kiba ambayo inakimbiza na kuwa trending namba moja.

 

Mwanadada anayetikisa kwenye anga la Bongo Fleva kwa sasa, Faustina Charles ‘Nandy’, ametisha vibaya mno baada ya kupiga pasi ndefu alipotoka na ngoma ya Na Nusu, basi ameachia mkwaju mwingine mkali wa Acha Lizame.

 

Nandy ameachia ngoma hiyo Juni 12, mwaka huu akiwa na mkali na Mkurugenzi wa Lebo ya Konde Music WolrdWide, Rajab Abdul ‘Harmonize’. Ndani ya saa chache tu imetazamwa mara laki nne kuelekea tano na kukamata trending namba mbili pale mjini YouTube.

 

Mwanzo mashabiki walianza kuhisi kuna kolabo inakuja kati ya Nandy na Harmonize au Harmo baada ya kuonekana wakiwa wanachati.

 

OVER ZE WEEKEND inakuletea usichokikua juu ya ngoma hii ya Acha Lizame;

Kabla ya kutoa video ya ngoma hiyo, mwanzo Nandy aliipigia promo kwa kuweka cover, akiwa anawaandaa mashabiki wake wakae mkao wa kula.

 

Nandy amekuwa akitoa ngoma baada ya ngoma na zote zikiwa kali, hajawahi kushuka kwenye chati kutokana na bidii na uzuri wa kazi zake.

 

KOLABO

Tukizungumzia kolabo ya ngoma hii, Nandy na Harmonize ni wasanii ambao wana fun-base (wafuasi) kubwa na vipaji vikali sana.

 

Kemistri hii imeweza kutengeneza kitu kikali sana, kwani wote ni wasanii wakali katika kuimba, kutumbuiza na wana mtandao mkubwa wa mashabiki kila pande ya Afrika.

 

Hii ni miongoni mwa kolabo ambazo zitakuwa kubwa sana na zinaweza kuweka historia kutokana na ukubwa wa majina ya wakali hawa wawili, kwani wote wana nyota ya kupendwa na mashabiki wa muziki mzuri.

 

Katika ngoma hii, Harmonize ‘Konde Boy’, amefanya kazi kali sana, kwani amefanya hata mwenye ngoma hiyo ambaye ni Nandy, kumwachia uwanja jamaa ili afanye yake.

 

UTUNZI

Acha Lizame, ni ngoma ambayo imepita katika kalamu za watunzi wakali ambao wamekuwa wakishiriki katika utunzi wa ngoma za Nandy.

Ngoma hii imeandikwa na J Melody, Logic na Harmonize mwenyewe.

 

Watunzi wawili; J Melody na Logic, wamekuwa wakihusika sana kwenye uandishi wa ngoma nyingi za Nandy ambazo zimekuwa zikifanya poa kunako soko la muziki wa Bongo Fleva.

 

Mbali na kuandikwa na waandishi hao wakali, pia imepita kwenye mikono ya producer anayefanya poa sana, Kimambo kutoka Studio za SOV. Mbali na ngoma hii, pia amehusika katika kutengeneza Ngoma ya Aibu ambayo ilifanya poa kwa wakati wake.

 

MAUDHUI

Ngoma hii kila mtu anaitafsiri kiaina yake, kutokana na jina la ngoma hiyo.

Acha Lizame, imezungumzia mapenzi, katika mashairi yake yamezungumziwa mapenzi.

 

Mwanadada anayemsifia mpenzi wake kwa sifa kedekede kutokana na mapenzi anayopewa.

Hata ukiisikiliza kwenye vesi ya pili jinsi Harmonize alivyoimba, aisee ni mashairi makali sana na ya kiufundi zaidi.

 

UBUNIFU

Video hii imepita kwenye mikono ya Director Elvis kutoka Studio za Rockshottz ambaye ametengeneza pia So Hot ya King Kiba na Bedroom Remix ya Harmonize.

Nandy amejiachia ile mbaya kwani ameonekana kuwa comfortable kwa kila kitu, kikubwa ambacho amefanya ni yale mauno ya hatari ndani ya video hii.

 

Lokesheni iliyotumika humo ni mazingira ambayo ni sahihi ingawa ni studio video, lakini kwa namna ambavyo yametengenezwa, imefanya hata rangi zisimchoshe mtazamaji.

 

Hata ukiangalia kwa upande wa mavazi, Nandy ameuza mno kwenye mavazi, ila kwa Konde Boy kama kawaida yake lazima avue shati, hiyo nayo imetosha kunogesha utamu wa video.

 

Miongoni mwa video kali za mwezi huu, video hii imetisha kwani director wake amefanya kazi kali. Ubunifu uliotumika ni balaa.

 

UCHANGAMFU

Ngoma hii imechangamka mno, kiasi kwamba unaweza kuitazama zaidi ya mara mia moja, ina vibe la kutosha.

Wasanii wenyewe wameonesha kuchangamka katika video jinsi inavyoonekana.

 

Harmonize ameonesha utundu wake kwenye kuimba, kwani ameimba kwa uhuru sana na kufanya ngoma inoge japo ameimba viitikio sana.

 

NANDY AFUNGUKA

Nandy amefunguka sababu ya kufanya kolabo na Harmonize katika ngoma hiyo, kwa kusema kuwa mapokezi ya ngoma hiyo ni makubwa.

 

“Mapokezi ya ngoma ni mazuri na makubwa mno, kwani ndani ya muda mfupi imetazamwa na watu zaidi ya laki nne kuelekea tano. Sababu kubwa ya kufanya kazi na Harmonize, ni msanii mzuri, haikuwa ngumu kukutana na kufanya naye kazi, mimi nina desturi ya kufanya kolabo na wasanii tofauti tofauti,” amesema Nandy.

 

HITIMISHO

Pongezi nyingi ziende kwa Nandy, kutokana na uzuri wa ngoma hii, kwani ameweza kuliteka tena soko kama ilivyo kawaida yake.

Hakika hajawahi kukosea, ni msanii wa kike wa Bongo Fleva ambaye anaipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania.

MAKALA: HAPPYNESS MASUNGA

Leave A Reply