The House of Favourite Newspapers

Kala: Madam Rita ni Mkombozi

0

STAA wa Hip Hop Bongo anayesumbua na ngoma zake za kiharakati, Jeremiah Masanja ‘Kala’, amesema hakuna kitu kinachomuuma kama kumsema vibaya Mkurugenzi wa Benchmark Productions na muasisi wa Bongo Star Search (BSS) Rita Paulsen ‘Madam Rita’.

 

Kala amesema Madam Rita amefanya kazi kubwa ya kuinua vijana ambao ndoto zao zilishazima kabisa.

 

Akistorisha na OVER ZE WEKEEND, Kala amesema kama kijana, amepata nafasi ya kuonekana kupitia BSS.

 

“Wanaweza kumuona Madam Rita wakajua ana pesa sana kumbe siyo hivyo wanavyofikiria, muhimu ni sisi vijana tuliopata nafasi kujiongeza na kutumia njia aliyotufungulia. Naweza kusema Madam Rita ni mkombozi wa vijana wengi,” amesema Kala.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply