The House of Favourite Newspapers

Balaa! Mapokezi ya Shigongo Uzinduzi wa Kampeni Buchosa – Video

0

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo, leo Ijumaa, Septemba 25, 2020, anazindua rasmi kampeni zake za kunadi sera zake na kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo ili waweze kumpa ridhaa ya kuwa mbunge kwa miaka mitano ijayo.

Wananchi wa Buchosa wamefurika katika Viwanja vya Mpira vya Nyakaliro kwa ajili ya kumlaki Shigongo na kusikiliza sera zake  ili wafanye maamuzi sahihi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Katika uzinduzi huo, Shigongo ameambatana na mkewe, Veneranda Ephraim, viongozi waandamizi wa CCM Wilaya ya Sengerema na Buchosa, Mgombea Ubunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘Msukuma’ pamoja na aliyewahi kuwa Mbunge wa Nyamagana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Marsha.

Licha ya mvua kubwa kunyesha tangu asubuhi ya leo Buchosa na Sengerema, lakini wananchi wa Buchosa wamefurika kuhakikisha wanamuunga mkono Shigongo na kusikiliza sera zake.

Leave A Reply