Kartra

Bale Kuanza Kukiwasha Premier Kesho

TOTTENHAM wanatarajiwa kuwa uwanjani kesho Jumapili kwa kukipiga dhidi ya West Ham United, ni mchezo wa Premier League na kuna taarifa kuwa Jose Mourinho anaweza kumpa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza staa wake, Gareth Bale.

 

Ikiwa Bale atapata nafasi ya kuichezea inamaanisha itakuwa ni mara yake ya kwanza kuanza kukipiga akiwa na jezi ya Tottenham tangu arejee klabuni hapo kwa mkopo msimu huu.

 

Winga huyo mwenye kasi, hajacheza mechi hata moja tangu asajiliwe kutokana na kuwa baada ya kutua kwa mkopo akitokea Real Madrid, alikuwa majeruhi kutokana na kuumia goti.

 

Bale amekuwa akifanya mazoezi kwa bidii kwa mwezi mmoja uliopita katika viwanja vya mazoezi vya timu yake hiyo, ikiwa atacheza itakuwa mara yake ya kwanza kuichezea Tottenham tangu alipofanya hivyo mwaka 2013.

 

Mourinho amekataa kuweka wazi kama atamtumia au hatamtumia alipokuwa akizungumzia mchezo huo.“Timu ni muhimu sana, Gareth yuko hapa kusaidia timu lakini wakati huo tunajali kuhusu afya yake.

 

Hivyo, maamuzi tutakayofanya itakuwa ni mazuri kwa timu na kwake pia.”Mashabiki wa Tottenham watakuwa wakisubiri kwa hamu kumuona Bale akianza katika kikosi hicho tangu alipoondoka kwenda Real Madrid kwa dau lililovunja rekodi wakati huo, pauni 85.3m mwaka 2013.

 

Tottenham kwa sasa ipo katika kiwango kizuri ikiwa imetoka kupata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford.


Toa comment