Banka Ageuka Tishio Yanga

KIWANGO cha juu cha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mohammed Issa ‘Banka’ ambacho hivi karibuni alikionyesha katika mchezo dhidi ya Simba, kimeonekana kumtisha Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime na kujikuta akisema kuwa watakuwa na kazi kubwa ya kufanya ili kumdhibiti.

 

Yanga itapambana na Kagera Sugar, Januari 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

 

Maxime ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga. Naamini utakuwa na ushindani mkubwa sana kwetu kutokana na jinsi wachezaji wa Yanga hivi sasa wanavyoonekana kuimarika, mfano mzuri ni Banka.

 

“Katika mechi mbili za hivi karibuni nilizomuona uwanjani, jamaa amerudi katika kiwango chake cha zamani, kwa hiyo inabidi tujipange kwelikweli kwani anaweza kuwa kikwazo kikubwa kwetu katika kutimiza malengo yetu, ninamfahamu vizuri na nimewahi kumfundisha nilipokuwa Mtibwa Sugar


Loading...

Toa comment