The House of Favourite Newspapers

Barabara ya Chato Kujengwa Upya

0

TAASISI ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita imemrejesha kujenga upya barabara ya Makurugusi kwenda Musasa wilayani Chato yenye urefu wa Kilometa 1.5 kwa gharama zake baada ya mkandarasi huyo wa kampuni ya M/S Runazi General Supplies Company LTD kudaiwa kujenga barabara hiyo chini ya kiwango na kusababisha barabara hiyo kuharibika vibaya siku chache baada ya kukamilika.

 

Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hiyo kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita, Leonidas Felix anasema wamelazimika kumrudisha katika eneo la ujenzi ili aweze kujenga barabara hiyo upya kwa gharama zake kutokana na kujenga chini ya kiwango na kusababisha wananchi kulalamika kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

 

ITV imezungumza na mkandarasi huyo Pancian Gasper akiwa katika ujenzi wa barabara hiyo nakusema barabara hiyo imeharibika mara baada ya kukamilika kutokana na kusombwa na mafuriko hivyo akalazimika kuijenga upya ili kutekeleza maagazo ya TAKUKURU.

 

Mhandisi wa TARURA wilaya ya CHATO Edgarevarist Kidasi amesema mkandarasi atakayebainika kujenga barabara chini ya kiwango atawajibika kujenga upya kwa gharama zake na kuchukuliwa hatua huku wananchi wakieleza namna wanavyopata adha ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara.

 

Leave A Reply