The House of Favourite Newspapers

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, (TEC) Wametoa wito Viongozi wao Kujikinga na Covid 19

0

BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania, (TEC) wametoa wito wa viongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu kujikinga na kupigana vita dhidi ya Covid 19 kuzingatia tahadhari zilizotolewa na wataalamu wa afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, mapema leo, Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu Tanzania, Padri Charles Kitima, amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kujuwa kwamba mtu anatakiwa kulinda uhai wake na wa mtu mwingine huvyo ni wajibu kila mtu kujikinga.

“Kila mmoja wetu wanatakiwa kujuwa jinsi ya kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na Wizara ya afya ili kuepuka vifo kwa viongozi wa dini na waumini na watanzania wote.

“24 Februari Waziri wa afya aliweka na kuhainisha tahadhari zinazotakiwa kufatwa ili kuepukana na ugonjwa huo, tutawasaidia kwa kuwapa ulinzi na msaada kwa kutokuwa chanzo cha maambukizi kwa kunawa, kuvaa barakoa na kukaa umbali unaozuia kuambukizana.

“Sisi kama viongozi wa dini, Kanisa katoliki Tumeshuhudia vifo vya mapadri wanaofanya kazi ya kuhudumia wangonjwa na wamepata tatizo hili la kupumua, lakini changamoto tunayoipata ni kuwa hatuwezi kuthibitisha kama ni Corona kwa kuwa hatuna vipimo hata kwenye mahospitali yetu tuna zaidi ya hospitali 500.

“Kwa kuwa sisi hatuelezwi na   madaktari, na hao madaktari  sio wote  wanaruhusiwa kupima na kuthibitisha kwa kuwa wizara imeweka utaratibu wake katika kutoa majibu lakini kwa kuwa vifo vinatokea kotekote tunawaomba Watanzania wachukuwe tahadhari.

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa kila Mtanzania amehusika kwa namna moja hama nyingine katika kushiriki msiba wa watu wanaokufa kwa tatizo la kupumua na mila zetu huwa wakina mama wanakuwa katika chumba kimoja cha mfiwa ili kumfariji bila kuwa na tahadhari hivyo basi ni vyema kuchukua tahadhari.

” Tumeona nchi nyingi zinapima na kusaidia watu kupata idadi ya wagonjwa na kuweza kuwasaidia hali inayoendelea inatutaka kuwasikiliza sana viongozi wetu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

“Viongozi tunapenda kushirikiana katika kupigania uhai wa watanzania kwa kila mtu kulinda uhai wake na uhai wa MTU mwingine kwa kupata taarifa za kiafya.

” Sasa ni wajibu wa kwa kuwa wanasayansi ni wakati wao wa kufanya uchunguzi kuhusiana na ugonjwa wa kupumua ili kuweza kupata taarifa kuhusu Watanzania.

“Ukweli unamuweka mtu huru, tuache kusema kuwa tukiwaambia ukweli watu tutakuwa na hofu hapana inatakiwa waambiwe ili wajuwe kuwa ni kitu cha kweli ugonjwa fulani unauwa.” amesema Kitima.

“Zaidi ya mapadri 25 wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa kupumua, masista zaidi ya 60, kwa miezi 3 mfululizo wakati si kawaida,huwa wanapoteza maisha lakini si kwa wingi huu kwa hiyo ifike mahali tuambiane ukweli kuwa Corona ipo na tunahitaji kuchukuwa tahadhari kwa hali ya juu kuhusiana na hili na hasa kipindi hiki cha sikukuu inayotarajiwa, amesema.

Leave A Reply