The House of Favourite Newspapers

Basata: Tumezuia Shoo Ya Nay Wa Mitego Kwa Sababu Amekataa Wito Wito Mara 2 – Video

0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema limetoa wito mara mbili kwa Msanii wa Bongo Fleva, Nay
Wa Mitego kufika Ofisini kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Wimbo wake wa Amkeni lakini hakutokea na hiyo ndio sababu ya kuzuia vibali vya kufanya shoo Mkoani Njombe

Mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha amesema “Tumempa wito kwa mara ya tatu afike Ijumaa hii (Septemba 8, 2023), tunasubiri kuona kama atafika au la, kuhusu kuitwa Polisi hayo hatuyajui, sisi tunadili na maadili ya Msanii.”

Awali, Mwanasheria wa Nay, Wakili Jebra Kambole akiongea na JamiiForums alisema “BASATA wamempa wito wa maandishi Nay afike ofisini kwao Ijumaa hii kwa sharti kuwa anatakiwa kwenda peke yake bila Mwanasheria, bado tunatafakari sharti hilo na kwa nini iwe hivyo.”

Leave A Reply