The House of Favourite Newspapers

Bashe Aagiza Aliyekamatwa na Kiwanda Bubu cha Mawese Asaidiwe

0

BAADA ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kufanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Halifani Issa (42) mkazi wa Kongowe Wilayani Kibaha kwa kosa la kumiliki na kuendesha kiwanda bubu cha kuchakata mafuta ya mawese bila ya kuwa na kibali kinyume na sheria.

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema wananchi kama hao hawapaswi kukamatwa kwani wanajitafutia kipato chao hivyo ni wajibu wa Serikali kuwasaidia badala ya kuwakamata na kuwaadhibu.

 

“Wananchi wanatafuta njia zao za kujipatia kipato, Halifani Issa anapaswa kusaidiwa kuonyeshwa njia za vibali na sio kukamatwa. Waziri wa Kilimo ndugu Hussein Bashe na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni kemeeni mambo haya. Huyu anafanya value addition. Support him,” amesema Zitto Kabwe.

Akimjibu Zitto, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amtafute Halfani na kumsadia kupitia SIDO, baada ya kuripotiwa kwa taarifa za kukamatwa kwake na Polisi Mkoani Pwani kwa kosa la kumiliki na kuendesha kiwanda bubu cha kuchakata mafuta ya mawese bila kuwa na kibali.

 

“Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh. DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia,” amesema Bashe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa wakati wa zoezi la kukamatwa kwa Halfani alisema wamemkamata yeye pamoja na madumu zaidi ya 90 yaliyojazwa mafuta ya mawese na akasema watashirikiana na Mamlaka nyingine za Serikali kama TMDA,TBS na OSHA ili kuweza kujua athari zinazoweza kupatikana.

Leave A Reply