The House of Favourite Newspapers

Ghana Yaondolewa AFCON 2021 kwa Aibu

0

TIMU ya Taifa ya Ghana imeondolewa rasmi kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 na timu ya taifa ya Comoros katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kwa kipigo cha goli 3-2 katika mchezo uliopigwa Jumanne Januari 18.

 

Ghana wakiwa kama washindi wa Kombe la Afcon mara nne wametolewa na timu ambayo ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo mikubwa ngazi ya mataifa Afrika.

 

El Fardou Ben Nabouhane aliipa uongozi Comoros mapema ikafuatiwa na kadi nyekundu ya moja kwa moja iliyotolewa kwa mchezaji mashuhuri Andre Ayew.

 

Ahmed Mogni aliongeza bao la pili kwa wageni wa michuano Comoros kabla ya Ghana Black stars kupambana na kurudisha bao hizo na matokeo kuwa 2-2.

 

Hata hivyo, wakati dakika zikielekea jioni Ahmed Mogni alifunga goli la tatu kwa Comoros timu ya Visiwani ambayo inashika nafasi ya 132 kwenye viwango vya Fifa bao ambalo limefanya rekodi ya tangia mwaka 2006 kuvunjwa rasmi.

 

Ghana ilianza kwa matokeo ya kusuasua kwenye mashindano haya ambapo walianza na kipigo cha kufungwa goli 1-0 na Morocco kabla ya kutoa sare ya bao 1-1 na Gabon.

Leave A Reply