The House of Favourite Newspapers

Batman Kuingia Sokoni Machi 4

0

The Hollywood Reporter imethibitisha kuwa filamu mpya ya Batman inayotarajiwa kutoka Machi 4, 2022 itakuwa na urefu wa saa 2 na dakika 55 ikiwa na dakika 8 za Credits.

 

Filamu hii iliyoongozwa na director Matt Reeves inaweka rekodi ya kuwa miongoni mwa filamu ndefu zaidi ya Super Hero kwenye Big Screen na ndefu zaidi kwa filamu za Batman.

 

Filamu ndefu zaidi ya Super Hero inashikiliwa na filamu ya Zack Snyder, Justice League yenye saa 4 na dakika 2 ila baadae ilipunguzwa na kuwa na Saa 2 kwaajili ya Cinema, Filamu nyingine ndefu zaidi ya Super Hero ni ya Marvel, Avengers: Endgame yenye Saa 3 na dakika 1 kwenye Big Screen.

 

The Batman imechezwa na Robert Pattinson kama Bruce Wayne na Colin Farrell kama adui Oswald ‘Oz’ Cobblepot aka The Penguin.

Leave A Reply