The House of Favourite Newspapers

Jay Z, Robin Thicke, Kelly Rowland, Meek Mill Waungana

0

Jay Z na wasanii wengine, akiwemo Robin Thicke, Kelly Rowland, Meek Mill, wamejitokeza na kuomba marekebisho sheria ya New York ili maneno ya nyimbo za rap yasitumike tena kama ushahidi wa uhalifu mahakamani.

Wasanii kadhaa walitia saini barua kuwataka wabunge wa jimbo la NY kuunga mkono marekebisho yaliyopendekezwa ambayo yatalenga kudumisha uhuru wa kujieleza katika muziki wa rap.

Wakili wa Jay-Z, Alex Spiro ameongea na Rolling Stone nakusema “Tumesubiri kwa muda sana, Kwa kubadilisha sheria hapa, unafanya mengi mazuri, lakini pia unatuma ujumbe kwamba maendeleo yanakuja. Tunatarajia mabadiliko haya kwenye miji mingine”.

Sheria ya Rap Music on Trial, iliwasilishwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana, mabadiliko haya yatawazuia waendesha mashtaka kutaja mashairi ya msanii flani kama ushahidi, isipokuwa ikiwa kuna ‘uthibitisho wa wazi na wa kusadikisha’ kwamba maneno hayo yanahusishwa na uhalifu.

Leave A Reply