The House of Favourite Newspapers

Bella kufanya video na Koffi mwakani

0

Stori: Andrew Carlos
Kimataifa zaidi! KING of the Best Melodies, Christian Bella amefungukia video ya ngoma yake ya Acha Kabisa aliyofanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide kuwa lazima akatengenezee nje ya nchi mwakani.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Bella aliwataka mashabiki wake waendelee kuupakua wimbo huo mtandaoni na kwamba video yake itakuwa sapraizi kubwa.

“Kwa mara ya kwanza nitaachia ngoma zangu mbili mpya kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya (Desemba 31, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live (Mbagala-Zakhem jijini Dar),” alisema Bella.

Leave A Reply