The House of Favourite Newspapers

Guus Hiddink achukua mikoba ya Mourinho Chelsea

0

Football - Tottenham Hotspur v Chelsea Barclays Premier League - White Hart Lane - 21/3/09 Chelsea manager Guus Hiddink Mandatory Credit: Action Images / John Sibley Livepic NO ONLINE/INTERNET USE WITHOUT A LICENCE FROM THE FOOTBALL DATA CO LTD. FOR LICENCE ENQUIRIES PLEASE TELEPHONE +44 (0) 207 864 9000.

Kocha mpya wa Chelsea, Guus Hiddink.

Aliyekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Guus Hiddink ameteuliwa kuwa kaimu meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu huu.

Hiddink ameteuliwa baada ya Jose Mourinho kutimuliwa Alhamisi iliyopita.

“Nimefurahia kurejea Stamford Bridge. Chelsea ni moja ya klabu kubwa duniani lakini haipo pale inakofaa kuwa kwa sasa. Hata hivyo nina uhakika tunaweza kubadilisha mambo,” amesema Hiddink baada ya kuteuliwa.

“Nasubiri kwa hamu kufanya kazi na wachezaji na wakufunzi wenzangu wapya katika klabu hii kubwa na kufufua uhusiano wangu mzuri na mashabiki wa Chelsea.”

Guus-Hiddink

Mholanzi huyo alikuwa uwanjani Stamford Bridge kutazama mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland ambayo ilisimamiwa na Steve Holland akisaidiwa na Eddie Newton, ambaye sasa atakuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

Hiddink, aliwahi kuinoa Chelsea wakati mmoja, alipowasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hajatia saini mkataba.

Hiddink alishinda mataji sita ya Ligi ya Uholanzi na Kombe la Ulaya akiwa meneja wa PSV Eindhoven ya Uholanzi katika vipindi viwili.

Pia aliongoza Timu za Taifa za Korea Kusini, Australia na Urusi kabla ya kujiunga na Chelsea mara ya kwanza kujaza pengo lililoachwa na Luiz Felipe Scolari Februari 2009.

Alijiuzulu wadhifa wake kama mkufunzi wa timu ya Taifa ya Uholanzi mwezi Juni, baada ya kutofanya vyema katika juhudi za kuwasaidia kufuzu kwa Euro 2016.

Leave A Reply