The House of Favourite Newspapers

Benki ya Exim Yaibika Kinara Uhifadhi Mazingira

0
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Lameck Charles (Kushoto) akipokea tuzo maalum kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija baada ya benki hiyo kuibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam katika serehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam hii leo.

Benki ya Exim imeibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam na hivyo kukabidhiwa tuzo maalum ya kutambua jitihada hizo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Tuzo hiyo maalum imekabidhiwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Amosi Makala katika serehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa tuzo iliyotolewa na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa Benki ya Exim baada ya benki hiyo kuibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam katika serehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam hii leo.

Kupitia mkakati wake wa kutunza na kuhifadhi mazingira unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ benki hiyo imekuwa mstari mbele katika kampeni mbalimbali za kuhifadhi mazingira ikiwemo upandaji miti ambapo hivi karibuni benki hiyo kwa kushirikiana na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ilipanda miti 10,0000 jijini Dodoma

Aidha, benki hiyo pia imekuwa imekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa bustani mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya majiji hapa nchini ikiwemo Dar es salaam.

Leave A Reply