The House of Favourite Newspapers

Kumekucha! Tazama Zari Alichomfanyia Babu Tale

0

IKIWA ni saa chache baada ya kutua Bungeni na ku-make headlines za kutosha, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amemmwagia sifa kama zote, mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Meneja wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’.

 

Sifa hizo amemmwagia Babu Tale baada ya kukutana naye jana Bungeni jijini Dodoma alipokuwa amekwenda kwa mualiko wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro. Zari ambaye alitambulishwa Bungeni kama balozi wa hiari wa utalii nchini aliandika ujumbe huu chini ya picha yake akiwa na Babu Tale.

 

“Mwanadamu mwenye malengo anaweza kubadilisha rangi za nguo, nyumba ya kuishi hata anaweza kubadili muonekano wa mwili wake lakini sio TABIA YAKE.

 

Asante Godfather Tale, jana ndio nilipata muda wa kufanya mazungumzo na wewe japo kwa uchache tangu umepewa dhamana ya kuwa Muwakilishi wa Wanamorogoro Kusini Mashariki (Mbunge).

 

Jambo kubwa lililonipa faraja ni kwamba, nimekukuta GODFATHER TALE ni yuleyule, huja badilika, huna maringo. Nimefurahi kuona kuwa bado ni mwenye kutamani maendeleo kwa kila aliyekuzunguka.

 

Endelea na moyo huo ili ufikishe malengo ya watu wako na Taifa kwenye mafanikio makubwa @babutale

Credits:

@hotpot_tz

@erick.evarist

 

Leave A Reply