The House of Favourite Newspapers

NMB yazindua mfumo wa kisasa wa taarifa za mikopo

0

NMB-1Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo uliozinduliwa na Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB’s) kwa lengo la kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 .NMB -2Afisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) namna Benki ya NMB inavyoongoza katika utoaji wa mikopo kwa makundi mbalimbali.NMB -3Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela( kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker . Picha na Aron Msigwa.

Benki ya NMB imezindua mfumo wa kisasa wa kuhifadhi taarifa za wateja utakaotumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB’s) kwa lengo la kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wanaoomba mikopo kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na ilivyokuwa mwanzo kutokana na taarifa zao kuendelea kuwepo kwenye mfumo huo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker amesema kuwa mfumo huo utaiwezesha Benki hiyo kuwahudumia wateja wake katika matawi zaidi ya 170 yaliyoko nchi nzima kwa haraka zaidi.

” NMB tumekuwa tukiboresha mifumo yetu ya utoaji wa huduma ili kuwapatia wateja wetu huduma bora, kulingana na utendaji wa mfumo huu mteja wetu sasa atapata mkopo wake ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma ambapo ilichukua takribani wiki mbili mteja kupata mkopo wake”

Amesema kuwa Benki hiyo husshughulikia maombi ya mikopo zaidi ya 700 kwa siku na kuongeza kuwa kupitia mfumo huo wa kisasa taarifa za huduma ya utoaji wa mikopo ndani ya NMB, mishahara ya wafanyakazi inayopitia Benki hiyo, waombaji wadogo na Wakubwa wa mikopo hiyo ikiwemo wafanyabiashara na makampuni zitadhibitiwa kutokana na uwepo wa mifumo huo wenye uwezo wa kuchambua na kuweka kumbukumbu za wateja wanaoomba na kurejesha mikopo kwa haraka.

Aidha amesema kupitia matumizi ya Mfumo huo ( Simbuka) Benki ya NMB itaweza kufuatiliaji taarifa za wateja kwa ukaribu zaidi.

Kwa Upande wake Afisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols amesema kuwa Benki ya NMB inaongoza katika utoaji wa mikopo kwa makundi mbalimbali nchini kwa mikopo inayofikia shilingi Trilioni 2.2 kwa mwaka ambapo asilimia 25 ni mikopo midogo na asilimia 25 ni mikopo ya wateja wakubwa.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kiwango kikubwa cha riba kinachotolewa na Benki za Tanzania ameeleza kuwa kinachangiwa na hali ukuaji wa uchumi wa eneo husika pamoja na gharama za kupata amana za mikopo na kutoa wito kwa mabenki kote nchini kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha utoaji wa huduma za kibenki nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo huo amesema umejengwa kwa ushirikiano na wataalam kutoka Nethaland,unawezesha ushirikiano wa taarifa za kibenki kutoka benki moja kwenda nyingine na sasa wateja watapata mikopo yao ndani ya siku 4 kutokana na taarifa za mifumo kuwasiliana.

Aidha, amesema mabadiliko hayo yameanzishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) yamechukuliwa kwa umakini na Benki hiyo kutokana na idadi kubwa ya mikopo na wateja inaowahudumia.

Aidha, amesema kuwa mtandao huo utasaidia Benki ya NMB kufuatilia na kubainisha mwenendo wa wateja wanaolipa vizuri na vibaya.

Leave A Reply