The House of Favourite Newspapers

Bernard Morrison Kuishtaki Yanga FIFA, Mtoa Taarifa Afunguka

0

 

Bernard Morrison

TAARIFA ambazo Championi Ijumaa zimepata ni kuhusiana na kiungo raia wa Ghana ambaye amepita Yanga na Simba, Bernard Morrison kutaka kwenda tena Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu kabisa na nyota huyo zimeeleza kuwa Morrison anaweza kwenda tena FIFA kuwashtaki Yanga kama wakishindwa kumpa stahiki zake ambazo anawadai.

Mtoa taarifa huyo alisema, ameambiwa na Morrison kuwa amewapa Yanga muda wa kuhakikisha kuwa analipwa fedha hizo na kama ikiendelea kuwa hivi ilivyo sasa, hatakuwa na jambo lingine zaidi ya kuomba msaada FIFA.

“Morrison amesema kuwa amewapa muda Yanga wa kuhakikisha kuwa wanamlipa fedha zake ambazo anadai, ingawa hajasema kuwa ni kiasi gani na fedha za nini.

“Kubwa amesema kuwa kama huo muda ambao ametoa hatolipwa ndiyo atakwenda FIFA ili aweze kupewa haki yake,” alisema mtu huyo.

Alipotafutwa Morrison mwenyewe ili kuweza kujibia taarifa hizo ilikuwa ngumu kumpata, ingawa mtu wake wa karibu alisema kuwa yupo Morocco kwenye klabu ya FAR Rabbat inayonolewa na Nasreedin Nabi akimalizia taratibu za kujiunga na timu hiyo.

Stori na Issa Liponda

Leave A Reply