The House of Favourite Newspapers

Best 20 Mastaa Waliokomba Mirahaba ya Nguvu COSOTA

0

SERIKALI ya Tanzania kupitia Chama cha Haki Miliki (COSOTA) imeanza zoezi la ugawaji wa mirabaha kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alitaka kuanzia Desemba, 2021 wasanii wawe wanalipwa kutokana na kazi zao kutumika kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo radio na TV.

 

Hata hivyo, katika ugawaji wa kwanza, nyimbo za Injili zimeonekana kupigwa na kusikilizwa zaidi katika vituo vya radio na runinga nchini hivyo kuwafanya waimbaji wa nyimbo za Injili kuibuka na vitita zaidi katika mgao wa mrabaha wa kwanza ulioanza kutolewa na COSOTA.

 

Kwaya Kuu ya Mtakatifu Cecilia Arusha imeibuka na mkwanja mzito wa Sh milioni 8.739 ikifuatiwa na Ali Saleh Kiba maarufu King Kiba ambaye ameupiga kwenye Bongo Fleva na kuchota Sh milioni 7.588 kutokana na mauzo ya nyimbo zake mbalimbali.

 

Wengine waliopokea mgao mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa ni Rose Mhando, Nandy, Saraphina, Ibraah na wengine wengi, lakini mjadala mkali ni juu ya staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz na wasanii wa lebo yake ya Wasafi kutotajwa ingawa hata Harmonize naye hajaoneshwa amepata kiasi gani.

 

COSOTA imetoa orodha ya Wasanii 21 wa Bongo Fleva ambao wameongoza kwa kupata pesa nyingi za mirabaha kutokana na nyimbo zao kuchezwa kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye Radio na TV ambapo nafasi ya kwanza imeshikwa na Alikiba.

1. Alikiba.
2. Ay
3. Ibraah
4. Harmonize
5. Diamond Platnumz
6. Mwana FA
7. Profesa J
8. Darassa
9. Juma Jux
10. Jay Melody
11. Mabantu
12. Nandy
13. Saraphina
14. Maua Sama
15. Anjella
16. Linah Sanga
17. Mwasiti
18. Luludiva
19. Abby Chamz
21. Ray C
20. Lady Jaydee.

Leave A Reply