The House of Favourite Newspapers

Prisons Wapo Tayari Kuwakabili Simba

0

LIGI Kuu ya NBC Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea jioni ya leo Alhamasi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambapo wenyeji Simba watapambana na Tanzania Prisons.

Timu hizo zinakutana huku zote zikiwa zimetoka kupoteza michezo yao iliyopita katika ligi kuu, Simba walifungwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Prisons walitembezewa kipigo cha mabao 0-4 dhidi ya Azam FC.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Ofisa Habari wa Prisons, Jackson Mwafulango, amesema: “Maandalizi yetu yamekamilika na wachezaji wako tayari kwa ajili ya mapambano yaliyo mbele yetu.”


Prisons mpaka sasa
wako katika nafasi ya 16 ambayo ndiyo ya mwisho katika msimamo wa ligi hiyo wakikusanya alama 11, huku Simba wakishika nafasi ya pili na alama zao 25.

STORI: DERICK LWASYE, MBEY

Leave A Reply