The House of Favourite Newspapers

Betika Latinga  Mbagala Kijichi, Mgeninani Lavutia Wazee wa Kubeti

0
Baadhi ya wasomaji wa Gazeti la Betika wa maeneo ya Mbagala Kijichi wakilisoma gazeti hilo.
MAPEMA leo Jumatano, Februari 19, mwaka huu timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Mbagala Kijichi, Mgeni nani jijini  Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi zaidi
Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wazee wa kubeti wameendelea kulisifia kwa ujio wake huo  kutokana na linavyowaapa ujanja wa kubet.
Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.
Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutangaza nalo.
Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.
Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.
Leave A Reply