The House of Favourite Newspapers

Betika Latua kwa Wafanyabiashara Kinyerezi, Tabata Segerea

0

MAPEMA leo Jumatano, Februari 5, 2020, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers imetembelea maeneo ya Kinyerezi, Tabata Segerea ambapo wafanyabiashara wa maeneo hayo wameonyesha furaha yao kulisoma Gazeti la Betika.

Wafanyabiashara hao wameonyesha furaha yao kukutana na timu ya maofisa masoko, wakidai kuwa wao pia mbali na kusoma habari za michezo ya kubeti pia wanapenda kutokelezea ndani ya gazeti hilo wakiwa kwenye biashara zao.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

 

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply