The House of Favourite Newspapers

BIEBER MAHAKAMANI KWA KUMGONGA MPIGAPICHA KWA GARI


MWANAMUZIKI maarufu wa Canada, Justin Bieber,  anashtakiwa kwa kumngonga na gari mpigapicha mmoja wakati akitoka kanisani mjini Los Angeles, Marekani,  mwaka 2017. mtandao wa The Blast umeripoti.

 

Mpiga picha huyo, William Wilson,  amesema alikuwa amesimama upande wa waenda kwa miguu  kabla ya ajali hiyo ambayo imemsababishia ulemavu na matatizo ya kisaikolojia

 

Hata hivyo,  mwimbaji huyo alijitetea akiwaambia waandishi waliokuwepo eneo hilo kuwa hakufanya hivyo makusudi bali ni kutokana na matatizo  ya kiafya aliyokuwa nayo siku hiyo.

Comments are closed.