The House of Favourite Newspapers

Black Rhino: Prof Jay Anaendelea Vizuri Muhimbili

0

KUFUATIA rapa maarufu na nguli wa Bongo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Mikumi Kupitia Chadema, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kuugua na kulazwa, familia yake imejitokeza kusema mkongwe huyo wa Muziki kwa sasa anaendelea vizuri huku wakiwaomba Watanzania waendelee kumchangia ili kufanikisha matibabu yake.

Kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, mdogo wa Prof Jay aitwaye Black Rhino amesema Jay anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Kaka mkubwa Prof. Jay anaumwa, kwa sasa yupo kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na anaendelea vizuri. Kama Familia tunaishukuru sana Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, madaktari bingwa wote, uongozi mzima wa Hospitali ya Muhimbili na manesi wanaomuhudumia laka mkubwa.

“Kwa kweli wanafanya kazi ya ajabu wanamuhudumia kwa upendo mkubwa sana na wanampatia huduma nzuri sana,” amesema Black Rhino.

Leave A Reply