Bocco: Banda Tuliza Akili

WINGA mpya wa kikosi cha Simba, Peter Banda amefunguka kuwa baada ya mazoezi ya jana Nahodha wa timu hiyo, John Bocco alimfuata na kumwambia atulize akili acheze mpira kwa sababu Wanasimba wana matumaini makubwa juu yake.

 

Banda amesema kitendo cha Bocco kumfuata na kuongea naye, kumemuongezea hamasa na hali ya kujiamini na anaamini kila kitu kitakaa sawa na ushindi utapatikana.

 

“Nahodha alikuja kuongea nami na kikubwa ameniambia niendelee kujituma na kutuliza akili kwa kuwa timu inahitaji ushindi na kwangu hilo ni jambo kubwa na linanifanya niongeze jitihada kila nitakapopata nafasi ya kucheza,” amesema.

 

Akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji, Banda amesema hakuna chochote kinachohitajika zaidi ya ushindi na wao kama wachezaji watajitahidi kuhakikisha hilo linafanikiwa na kuwapa mashabiki furaha.

 

“Tunahitaji kushinda kwenye mchezo wa kesho ni muhimu kwetu na wachezaji tunalijua tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunawapa mashabiki wetu furaha,” amesema Banda.


Toa comment