The House of Favourite Newspapers

Ufalme wa Tshabalala, Kapombe Wavunjwa Simba

0

ISRAEL Patrick Mwenda, nyota mpya ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, amefanikiwa kuuvunja ufalme wa beki wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na beki wa kulia, Shomary Kapombe uliodumu kwa muda mrefu kikosini hapo.

 

Mwenda ameibukia Simba akitokea KMC ambapo ujio wake ulikuwa unatajwa kukutana na ushindani mkubwa kikosini hapo kutokana na uwepo wa Kapombe na Tshabalala.

 

Akiwa na jezi ya Simba, katika mchezo wa kwanza wa ligi mbele ya Biashara United, Mwenda alianza kikosi cha kwanza na kufanikiwa kucheza kwa dakika zote 90, huku akionesha kiwango kikubwa.

 

Kipindi cha kwanza, Mwenda alicheza beki wa kushoto nafasi ya Tshabalala, ambapo muda wote aliweza kuwa mwiba kwa Biashara United ambapo alifanya majaribio manne na yote yaligota kwenye mikono ya kipa, James Ssetupa. Katika kipindi cha pili, Gomes alimtoa Kapombe na kuingia Tshabala ambapo ilimlazimu Mwenda ahamie beki wa kulia na Tshabalala kuchukua nafasi yake ya beki wa kushoto.

 

Aliyofanya Mwenda ilikuwa ngumu kufanywa na nyota wengine wa Simba ikiwa ni pamoja na David Kameta ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo ndani ya Biashara United, mwingine ni Gadiel Michael ambaye bado yupo ndani ya Simba.

Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita katika mechi zote muhimu na ngumu za Simba, Kapombe na Tshabalala walikuwa hawakosekani kikosini kama wapo fiti, lakini msimu huu umeanza tofauti kutokana na uwepo wa Mwenda, hivyo amefanikiwa.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply