The House of Favourite Newspapers

Bocco: Tunawajua Vizuri Azam

0

MSHAMBULIAJI mkongwe na nahodha wa Simba, John Bocco ametamba kuwa anawajua vizuri wapinzani wao Azam FC, hivyo ni lazima wawafunge katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.

 

Mchezo huo umepangwa kupigwa leo saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan huko Unguja ambao lazima wapate ushindi ili watinge hatua ya fainali.

 

Huo utakuwa mchezo wake wa nne Bocco kucheza tangu arejee uwanjani akitokea kwenye majeraha baada ya kucheza miwili ya Ligi Kuu Bara na mmoja wa Kombe la Mapinduzi walipocheza na Zimamoto na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1.

 

Bocco amesema kuwa katika mchezo huo wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili wafike fainali na kulichukua kombe hilo linalotetewa na Azam FC.

 

Bocco alisema kuwa siyo Kombe la Mapinduzi pekee wanaloliangalia, pia wanayaangalia makombe mengine yote wanayoshiriki na kikubwa ni kuyachukua ili kutengeneza rekodi ya timu yao.

 

“Tunataka ushindi ili tufike fainali na tuchukue Kombe la Mapinduzi, siyo hilo pekee, tunataka kuchukua kila kombe litakalokuwepo mbele yetu na hilo linawezekana kwao.

 

“Azam timu nzuri tunawajua vizuri, ninaamini na wao wanatujua lakini timu itakayofanya maandalizi mazuri ndiyo itakayopata matokeo mazuri ya ushindi.

 

“Tunaangalia upungufu wetu uliojitokeza kwenye mchezo wetu uliopita ili tuurekebishe na mwisho wa mchezo tupate ushindi, hivyo ninaamini kocha ameona upungufu wetu ataufanyia marekebisho ili tupate matokeo mazuri,” alisema Bocco.

Leave A Reply