The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Mikopo Kufuta Tozo kwa Wanufaika

0

SERIKALI imesema kuwa kuanzia Julai mosi mwaka huu Bodi ya Mikopo (HESLB), itafuta tozo ya asilimia 6 ya kulinda thamani ya fedha inayotozwa kwa wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

 

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 25, 2021, Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Juma Omary Kipanga wakati akijibu swali la mbunge wa Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa lililohoji ni lini serikali itapeleka Bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ya mikopo ya elimu ya juu.

 

“Kuanzia Julai 1, 2021, Bodi ya Mikopo itafuta tozo ya 6% ya kulinda thamani ya fedha inayotozwa kwa wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

 

“Vilevile itatekeleza maelekezo yangu ya kuondoa tozo ya asilimia 10 kwa wanufaika wanaochelewa kurejesha mkopo baada ya muda wa miezi 24 kupita baada ya kuhitimu,” amesema Naibu Waziri Mhe. Kipanga akijibu swali hilo.

Leave A Reply