The House of Favourite Newspapers

Bondia ‘Marvelous’ Afariki Dunia

0

Bingwa wa zamani wa dunia wa uzito wa kati Marvin Hagler ‘Marvelous’ amefariki akiwa na umri wa miaka 66. Raia huyo wa Marekani alitawala ngumi za uzito wa kati kutoka 1979 hadi 1987.

 

 

Katika wakati huo Hagler alipigana mapambano 67, akishinda 62 huku 52 ikiwa ni kwa KO. Sare mara 2 na kupigwa mara 3.

 

“Leo, kwa bahati mbaya mume wangu mpendwa Marvelous Marvin amefariki bila kutarajia nyumbani kwake hapa New Hampshire,” amethibitisha mkewe Kay Hagler.

 

 

Ikumbukwe mnamo Septemba 1980, Hagler alipambana na Alan Minter wa Uingereza kwenye Uwanja wa Wembley kupambania mataji yake ya kwanza ya Ulimwengu na akashinda mikanda ya WBA na WBC.

Leave A Reply