The House of Favourite Newspapers

Uthamani wa Muvi ni Uhalisia

0

Na Salum Milongo/GPL

Neria ni filamu ya Zimbabwe aliyochezwa mwaka 1993, iliyoandikwa na mwandishi Tsitsi Dangarembga. Filamu hii iliyoongozwa na Godwin Mawuru na kwa kushirikiana na Louise Riber. Ni filamu ya juu kwa hadhi katika historia ya Zimbabwe.

Filamu hii inayohusu mapambano ya mwanamke katika kitongoji cha mji mkuu, Harare, nchini Zimbabwe. Ujumbe wa Filamu hii ni kwa wanawake wajane.

Baada ya mwanaume kufariki dunia kwa ajali ya gari, mwanamke anabaki na watoto na ndugu wa mume wake wanatazama mali na kuitupa familia ya marehemu mdogo wao.

Filamu imechezwa vizuri kwa uhalisia hakuna vipodozi na ushindani wa sura nzuri na mavazi kama ilivyo desturi kwa filamu za hapa nyumbani.

Wimbo uliyosikika katika filamu hiyo, uliimbwa na muimbaji maarufu nchi Zimbambwe, Oliver Mtukudzi ulikuwa ukiongeza uhalisia kwani wimbo huo uliimbwa kiafrika.

Filamu za Bongo Muvi, hakuna muvi yenye ya kitaifa, hakuna filamu inayohifadhi. Miaka kumi baadae hatutakuwa na filamu ya kumuonyesha mtoto wa zama hizo.

Bado wachezaji wanalalamika filamu haziuzi, filamu ya Neria mpaka leo hii bado inauza mtandaoni. Ni kweli kabisa wala sisemi uwongo filamu za Bongo Muvi zimekosoa uhalisia.

Filamu zinachezwa hotelini, sisi maisha yetu si ya hoteli. Tunahitaji filamu inayoonyesha matatizo yetu na utatuzi wake, filamu zijibu maswali magumu yaliyopo mtaani sio kutuonyesha mavazi na aina ya vipodozi.

Mtu anamka asubuhi lakini usoni amepaka kila aina ya poda hili halikubaliki na muvi hazitauza kwa namna hiyo, kwa maoni na ushauri nitumie ujumbe whatsaap 0652262797

 

Leave A Reply