The House of Favourite Newspapers

Bossou Ndiyo Basi Tena Yanga

0

Sweetbert Lukonge | CHAMPIONI JUMNATATU| Dar es Salaam

KIKOSI cha Yanga, juzi Jumamosi kilifanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la FA baada ya kuitandika Prisons ya jijini Mbeya mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati wapenzi na mashabiki wa Yanga wakisherehekea ushindi huo, hofu kubwa imetanda kwenye benchi la ufundi la kikosi hicho baada ya kupokea ripoti kuwa beki wao wa kati, Mtogo, Vincent Bossou atakuwa nje ya uwanja kwa muda.

Bossou anasumbuliwa na maumivu ya goti ambalo aliumia wakati timu hiyo akijiandaa na mechi ya marudiano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ambayo ilifanyika nchini Algeria, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kusafiri na kikosi chake kwa ajili ya mechi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema kuwa baada ya Bossou kufanyiwa vipimo hivi karibuni, imegundulika kuwa ana jeraha kubwa ambalo litamfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Kutokana na hali hiyo hivi sasa anaendelea na tiba huku akitakiwa kupumzika kwa muda mrefu kidogo bila ya kufanya kazi yoyote ngumu ambayo inaweza kusababisha asipone haraka.

“Hata hivyo, wachezaji wengine wote waliokuwa majeruhi wanaendelea vizuri na Mungu akipenda kesho (leo), Justin Zulu ataanza mazoezi ila Donald Ngoma anaweza kuanza baada ya siku tatu au nne hivi kwani kwa sasa anaendelea vizuri,” alisema Bavu.

Mwanariadha Mtanzania Simbu Avunja Rekodi Nyingine England Marathons

Leave A Reply