The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Bongo Muvi Kuandamana… Nay wa Mitego, Mlela Hapatoshi

0

NA: GLADNESS MALLYA | IJUMAA WIKIENDA | OVER THE WEEKEND

BAADA ya wiki iliyopita mastaa wa filamu kuandamana kupinga uuzaji holela wa filamu za nje ya nchi kwa sababu zinawaharibia soko, hali imekuwa tete kwa msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na muigizaji Yusuf Mlela kutokana na kutoleana maneno makali, Wikienda lina data kamili.

Akizungumza na Wikienda, Nay alisema anawashangaa wasanii wa filamu kuandamana kisa filamu za nje wakati zilianza kuuzwa hata kabla wao hawajafikiria kuanza kuigiza hivyo wanatakiwa kufanya kazi nzuri zenye ubunifu na siyo vinginevyo.

Nay wa Mitego.

“Nawashangaa sana Bongo Muvi kuandamana, muvi za nje zipo tangu enzi na enzi hata kabla wao hawajaingia kwenye sanaa hiyo, wanatakiwa kufanya kazi maana wamekosa ubunifu pia waache upuuzi,” alisema Nay.

Baada ya Nay kuzungumza hayo Mlela naye alimjibu kwa kumwambia kwamba anatakiwa kukaa kimya kwani wanachofanya wanatetea haki yao kwani Nay alikuwa chokoraa tu lakini sasa amefanikiwa ndiyo anaongea maneno yasiyofaa kwa kuwaita wapuuzi.

Nay alijibu tena na kuliambia Wikienda kwamba anakubali ni kweli kwamba alikuwa chokoraa lakini sasa hivi ni tajiri je, huyo Mlela ana kitu gani cha kumfikia, anamshangaa kwa kuwa yeye aliuliza tu nani aliyewapa wazo la kuandamana na kwamba wanatakiwa kuwa wabunifu.

Msanii Yusuph Mlela ‘Angelo’

Kwa mara nyingine Mlela alijibu kwa kusema; “Nay yeye akae na utajiri wake isiwe ndiyo kigezo cha kumfanya aongee anachojisikia, maisha siyo pesa, maisha ni kuishi kwa kuheshimiana na wenzako hata kama wewe ni tajiri, sina bifu na Nay mimi nilimjibu kwa hiyo chochote anaweza kuamua maana aliongea ili ajibiwe na nilimjibu na maamuzi yangu ndiyo yale.”

Pamoja na wasanii hao kutofautiana wengine waliokerwa na tukio la kuandamana kwa baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi ni Mwanamuziki Isabela Mpanda aliyekiri kukerwa sana kwani walitakiwa kufanya kazi nzuri ziuzike siyo kuingiza mambo ya kisiasa.

“Tumekuwa watu wazima jamani tunatakiwa kubadilika, mmeshaona wapi au nchi gani wakiandamana eti kazi zetu zisiingie kwao kama siyo ujinga huo?

Tuache kiki za kipumbavu, kama ilikuwa inatafutwa haki kweli kwa nini tusingeungana Bongo Fleva na Bongo Muvi tukaandamana, tuache siasa tufanye kazi,” alisema Isabela.

Maneno aliyoyaandika Yusuf Mlela.

ILIKUPITA HII YA BONGO MUVI KUANDAMANA?

Leave A Reply