The House of Favourite Newspapers

Bozi apunwa simu kwenye kamari

0

Fatuma-Ayubu-‘Bozi’.jpgStori: Mayasa Mariwata

AMEPUNWA! Ndivyo wasemavyo watoto wa mjini kufuatia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ’Bozi’ kuambulia maumivu baada ya ‘kuliwa’ simu yake aina ya Samsung yenye thamani ya shilingi laki tano alipoenda kucheza kamari maeneo ya Kariakoo jijini Dar.

Mtoa ubuyu wa kujitegemea alivujisha kuwa, msanii huyo ni kawaida kucheza michezo hiyo ambapo siku hiyo alifika akiwa na bashasha tele kwa lengo la kuibuka kidedea, cha kustaajabisha mshindi alipoibuka mwingine na yeye kutakiwa kutoa shilingi laki moja,  mfukoni hakuwa na kitu ndipo akapokonywa simu yake.

Baada ya ubuyu huo kutufikia na Bozi kutafutwa alisema; Dah!  Ni kweli nimelizwa ni jambo la kawaida kwenye kamari, kushinda au kupoteza so hakuna tatizo vitu vidogovidogo kama hivyo ni vya kutafuta tu!”

Leave A Reply