The House of Favourite Newspapers

Brazil: Bolsonaro Apigwa Marufuku Kuwania Urais kwa Miaka Minane

0
Jair Bolsonaro

Mahakama ya Juu Zaidi ya Uchaguzi nchini Brazil imepiga kura kumzuia aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro kuwania kiti hicho kwa miaka minane.

Bw Bolsonaro alipatikana na hatia ya kutumia mamlaka yake vibaya kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka jana.

Alikuwa ameshutumiwa kwa kuhujumu demokrasia ya Brazil kwa kudai kwamba mfumo wa kielektroniki uliyotumiwa ungeweza kudukuliwa na ulaghai.

Mawakili wa Bw Bolsonaro wanatarajiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Wamesema kuwa kauli zake hazikuwa na uhusiano wowote na matokeo ya uchaguzi.

SHAMSA FORD AMEJIBU -“MTOTO WA MUME WANGU ni WANGU, MIMI NDIYE MRS. HUSSEIN, IMESHAKUA”

Leave A Reply